New Post

Tuesday, July 26, 2022

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MRADI WA PMI-VECTORLINK TANZANIA kwa kushirikia na HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO

 
TO JOIN OUR TELEGRAM GROUP CLICK HERE

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

 

22/07/2022 MRADI WA PMI-VECTORLINK TANZANIA kwa kushirikia na HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO wanatangaza nafasi za kazi za muda mfupi kuanzia siku 1 – 35 kulingana na kazi husika. Mradi wa VectorLink Tanzania ni mradi unaohusika na upuliziaji wa kiuatilifu ukoko kwa ajili ya kuua mbu waenezao ugonjwa wa malaria majumbani. Mradi unahitaji kuajiri watumishi wengi wa muda mfupi ili kutekeleza zoezi hili katika halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Watumishi watakaohitajika watakuwa wa nafasi mbalimbali; ambao wamekidhi vigezo vilivyowekwa kulinganana majukumu ya kazi husika. Taratibu na mchakato mzima wa ajira utaratibiwa na Halmashauri ya Wilaya na kusimamiwa na watendaji walioteuliwa kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ambao ni Mratibu wa Malaria wa Wilaya, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Wilaya, Afisa Afya wa Wilaya, Mganga Mkuu wa Wilaya, Mwakilishi mmoja toka Taasisi ya kupambana na rushwa, pamoja na Usalama wa Taifa. Mradi wa VECTORLINK Tanzania utawajibika kutoa miongozo ya kitaalamu na kusimamia mchakato mzima. Utaratibu madhubuti utawekwa kuhakikisha mchakato huo unakuwa wa uwazi na wa haki. Usawa wa kijinsia utakuwa ni mojawapo ya kigezo katika

DOWNLOAD PDF HERE